Habari za Punde

HABARI NA MATUKIOKATIKA PICHA YANGA ILIVYOTINGA HATUA YA RORBO FAINALI FA CUP

Kipa wa Yanga Deogratius Munishi, akiruka kupangua mpira wa hatari langoni mwake wakati wa mchezo huo.
**********************************************
TIMU ya Yanga leo imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe Azam Sports Federation 'FA' la baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Kiluvya United ya mkoani Pwani katika mchezo wa kukamilisha hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Obrey Chirwa aliibuka kinara wamabao kwa kuifungia timu yake jumla ya mabao manne kati ya sita, mengine yakifungwa na viungo Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi. 
Baada ya ushindi wa leo Yanga sasa itakipiga na Tanzania Prisons katika Robo Fainali Machi 18, mwaka huu mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Robo fainali nyingine zitakuwa kati ya Simba SC na Madini FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Azam FC na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kagera Sugar na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Kaitaba. 
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa refa hodari anayechipukia nchini, Kheri Sasii, hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Winga Geoffrey Mwashiuya alianza kwa kufungua kapu la mabao katika dakika ya 11 kwa shuti kali baada ya kuwatoka na kuwazidi mbio walinzi wa Kiluvya United kufuatia pasi ya beki wa kushoto, Oscar Joshua.
Bao la pili likafungwa na Obrey Chirwa katika dakika ya 24 kwa shuti kali la guu la kushoto baada ya pasi nzuri ya kutanguliziwa na Juma Mahadhi. 
Alikuwa ni Edgar Charles, aliyeipatia bao la kufutia machozi Kiluvya katika dakika ya 40 akamtoka Vincent Bossou baada ya pasi ya Shala Juma na kumtungua kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ .
Chirwa akafunga tena mabao mawili katika dakika za 45 akimalizia pasi ya Juma Mahadhi na dakika ya 70 akimalizia krosi ya Hassan Kessy kukamilisha hat trick yake ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo Julai mwaka jana kutoka FC Platinums ya Zimbabwe.Juma Mahadhi akaifungia Yanga bao la tano dakika ya 74 kwa shuti la umbali wa mita 21 hadi misuli ikambana na kutolewa nje kwa machela na Yanga wakaamua kucheza pungufu hadi mwisho wa mchezo huo. 
Juma Mahadhi akitolewa nje kwa machela baada ya kuumia
Daktari wa Yanga akimhudumia Juma Mahadhi baada ya kuumia
Beki wa Yanga Oscar Joshua, akichuana na wachezaji wa Kiluvya Utd
Obrey Chirwa kiashangilia moja kati ya mabao yake
Chirwa akishangilia
Hassan Kessy akipiga krosi
Msuva akipiga krosi
Msuva akimtoka kipa wa Kiluvya
Chirwa akikabidhiwa mpira na mwamuzi wa mchezo huobaada ya kumalizika
Aliyekuwa Kocha wa Yanga Pluijm akipiga story na mashabiki wa Yanga baada ya mchezo kumalizika

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.