Habari za Punde

HASSAN KABUNDA MCHEZAJI BORA WA MWEI LIGI KUU BARA MWEZO FEBRUARI

Mchezaji wa timu ya Mwadui FC, Hassan Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Februari kwa msimu wa 2016/2017.
Kabunda aliwashinda wachezaji Laudit Mavugo wa Simba SC na Ibrahim Ajib pia wa Simba SC. 
Katika mechi tatu ambazo Mwadui ilicheza kwa mwezi huo, Kabunda alicheza kwa dakika zote 270 na kuisaidia timu yake kukusanya jumla ya pointi sita zilizoifanya ipande kwa nafasi mbili katika Msimamo wa Ligi kwa mwezi huo wa Februari (kutoka nafasi ya nane hadi ya sita).
Kabunda alifunga jumla ya mabao manne katika mechi hizo tatu kati ya sita iliyofunga timu yake. Kiungo huyo mshambuliaji alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la mdomo au kadi kutoka kwa waamuzi.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Kabunda atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.