Habari za Punde

KADI NYEKUNDU YA OBREY CHIRWA YAFUTWA, MWAMUZI KUJADILIWA


Na Mwandishi Wetu,Dar

Mshambuliaji wa Yanga aliyezawadiwa kadi nyekundu wakati wa mchezo dhiri ya Ruvu Shootingi siku ya Jumatano wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Obrey Chirwa afutiwa rasmi kadi hiyo, huku mwamuzi alimnyima bao la wazi na kumpa kadi hiyo akiitwa ili kujitetea baada ya leokujadiliwa na endapo ataonekana ana makosa basi atafungiwa kuchezesha.
Akizungumza na Mtandao huu msemaji wa TFF Alfred Lucas alisema kuwa Bodi hiyo imemfutia kadi moja ya njano Chirwa ambapo 'Automatical' Kadi nyekundu inakuwa imejifuta.
Kwa maamuzi hayo ya Kamati ya Bodi ya Ligi ya TFF, sasa Chirwa yupo huru kukipiga katika mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Suga katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhurimjini Morogoro baada yakamati hiyo kujiridhisha kuwa kadi hiyo ilitolewa kimakosa kwa mchezaji huyo.
“Kadi ya Chirwa imefutwa kufuatia Yanga kuwasilisha malalamiko dhidi ya mwamuzi Ahmada Simba wa Kagera. Na Bodi imejiridhisha kwamba mwamuzi huyo alipitiwa, hivyo kuifuta kadi hiyo na sasa yuko huru kuichezea timu yake katika mchezo ujao,”amesema Ofisa mmoja wa Bodi ambaye hakutaka kutajwa jina. 
Chirwa alionyeshwa kadi mbili za njano za utata ndani ya dakika mbili na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 katika mchezo ambao Yanga ilishinda 2-0.
Alionyeshwa kadi ya kwanza ya njano dakika ya 44 baada ya kuifungia Yanga bao safi ambalo lingekuwa la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Hassan Kessy, lakini mwamuzi Ahmada Simba wa Kagera akalikataa na kumuonyesha kadi ya njano.
Na Mzambia huyo akaonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 45 baada ya kuudunda mpira chini na kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mapema dakika ya 31 Chirwa alifumua shuti kali langoni mwa Ruvu, ambalo lilimbabatiza mkononi beki Damas Makwaiya na Simba akaamuru mkwaju wa penalti, uliotiwa nyavuni na Simon Msuva kuipatia Yanga bao la kwanza.
Yanga ilipata bao lake la pili kupitia kwa Emmanuel Martin dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida akimalizia kwa kichwa krosi ya Simon Msuva kutoka upande wa kulia.
Yanga imeondoka leo Alfajiri Dar e Salaam kuelekea Morogoro tayari kwa mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.