Habari za Punde

KAMPUNI YA QUALITY GROUP YAWEKA WAZI DHAMIRA YAO YA KUKUZAKIPATO CHA WATANZANIA

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KAMPUNI ya Quality Group leo imeweka wazi mikakati yake ya kuendelea kukuza kipacho cha wananchi wa Tanzania kwa kujikita katika sekta mbalimbali zikiwemo za madini, kilimo cha sukari na kuanzisha Kiwanda ili kuendelea kutoa ajila pamoja na usambazaji wa  matrekta nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Kampuni hiyo, zilizopo Barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni hayo Nicholaus Raphl, alisema kuwa
Kampuni ya Quality toka ilipoanzishwa nchini imeweza kuajiri wafanyakazi zaidi ya laki sita (667,300) huku ikitoa ajira zaidi kwa kuwaajiri wazawa.
Aidha Quality Group katika kukuza sekta ya viwanda nchini imeingia mkataba na kampuni ya Solanika International Tractors Limited, ambapo mradi huo utaanza kwa mkoa wa Morogoro kwa takribani matreka 1000 na kusema kuwa jumla ya watanzania 1200 watapata ajira katika mradi huu unao tarajia kukamilika mwaka 2018.
Uanzishwaji wa mradi huo utawasaidia watanzania kupata matreka yenye ubora na bei nafuu kutokana na kuwa Matreka hayo yatakuwa yakitengenezwa nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Solanika.
Pia, Raphl alisema kuwa Quality wamedhamiria kuwekeza zaidi katika sekta ya afya kwa kujenga vituo 4,000 vya afya nchini, ambavyo vitawawezesha wananchi kupata huduma za kiafya kwa urahisi zaidi mbapo tayari kampuni kutoka nchini Urusi wameingia makubaliano ya kusambaza dawa kwenye vituo hivyo.
Mbali na hayo, pia Quality wameweza kujikita katika kukuza elimu ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali wa uvuvi kwa wananchi wanaoishi kando ya Ziwa Victoria na kuwapatia vifaa vinavyostahili kwa kutumika kwenye uvuvi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.