Habari za Punde

MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO WA SERIKALI WATOA MSAADA SHULE YA MSINGI BUIGIRI WASIOONA

 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi Zamaradi Kawawa akikabidhi moja ya mashine za nukta nundu kwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri iliyopo Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi Zamaradi Kawawa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri iliyopo Mkoani Dodoma wakati Maafisa Mawasilaino serikalini walipoenda kutoa msaada Shuleni hapo wenye thamani ya Sh Mil 12 zikiwemo mashine za nukta nundu na karatasi maalum.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bibi Sylivia Lupembe akitoa neno kwa niaba ya wanachama wa TAGCO kabala ya kukabidhi msaada Shuleni hapo wenye thamani ya Sh Mil 12 zikiwemo mashine za nukta nundu na karatasi maalum.
 Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Buigiri Samwel Jonathan akisoma risala kwa wageni Maafisa Mawasiliano kabla ya kupokea msaada kutoka Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) wenye thamani ya Sh Mil 12 zikiwemo mashine za nukta nundu na karatasi maalum.
 Mmoja ya Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri Joseph Richard akitoa neno la shukrani kwa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) mara baada ya kupata msaada wenye thamani ya Sh Milioni 12 zikiwemo mashine za nukta nundu na karatasi maalum.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri wakiimba wimbo maalum wa kuwakaribisha wageni kutoka Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) walipowatembelea na kuwapa msaada wenye thamani ya Sh Milioni 12 zikiwemo mashine za nukta nundu na karatasi maalum.
Baadhi ya Maafisa Mawasiliano Serikalini wakiwasikiliza wanafunzi wa Msingi Buigiri wakiimba wimbo maalum wa kuwakaribisha Shuleni hapo walipowatembelea na kuwapa msaada wenye thamani ya Sh Milioni 12 zikiwemo mashine za nukta nundu na karatasi maalum.   Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.