Habari za Punde

MAFURIKO YAZUA TAFRANI MAENEO YA JANGWANI NA KIGOGO, MMOJA AHIFIWA KUFA KWA KUSOMBWA NA MAJI

Baadhi ya Nyumba zilizopo Mitaa ya Jangwani zikiwa zimezama majini kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar esSalaam, leo asubuhi. Imeelezwa kuwa katika mafuriko hayo mtu mmoja amefariki dunia kwa kusombwa na maji.
 
Baadhi ya watu akiwa eneo hilo wakishuhudia maji hayo yaliyokuwa na kasi ya ajabu.
Baadhi ya Kinamama walilazimika kuwafuata watoto wao mashuleni baada ya kuona maji hayo yakizidi kuwa mengi na kukatisha barabara.
Baadhi ya Kinamama walilazimika kuwafuata watoto wao mashuleni baada ya kuona maji hayo yakizidi kuwa mengi na kukatisha barabara.
Vijana wakihamisha bidhaa katika maduka yaliyopo eneo hilo
Magari yakipita kwa taabu eneo hilo
Magari yakipita kwa taabu eneo hilo
Raia wa Kigogo wakiwa wamewahi kuokoa baadhi ya vitu vyao ndani ya majumba hayo yaliyojaa maji.
Baadhi ya nyumba zilizopo mitaa hiyo ya Kigogo.
Wakazi wa Kigogo wakiwa nje na vitu vyao walivyowahi kuokoa katika majumba yao.
Wakazi wa Kigogo wakiwa nje ya nyumba zao baada ya kujaa maji.
Wakazi wa Kigogo wakiwa pembezoni mwa barabara na mizigo yao waliyowahi kuokoa.

Maji hayo yakiwa yamejaa hadi usawa na ukingo wa Daraja.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.