Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA, ANNE MAKINDA, MAMA SOFIA SIMBA WAHANI MSIBA WA KAHAMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha maombolezo cha Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya kwanza, Balozi Sir George Kahama ,nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam leo mchana. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimfariji mjane wa Marehemu Sir George Kahama Janeth Kahama, nyumbani kwake Mikocheni B. jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa UWT aliyeng'atuka hivi karibuni, Sofia Simba, akisaini Kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Sir George Kahama, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Mikocheni B jijini Dar es Salaam,jana kwa ajili ya kutoa pole. 
 Sofia Simba, akimfariji mjane wa Marehemu Sir George Kahama Janeth Kahama, nyumbani kwake Mikocheni B. jijini Dar es Salaam
 SPIKA wa Bunge mstaafu, Anne Makinda akisaini Kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Balozi Sir George Kahama,  wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Mikocheni B jijini Dar es Salaam,leo mchana kwa ajili ya kutoa pole. 
 Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda (kushoto) akimfariji mke wa marehemu Balozi Sir George Kahama, Mama Janeth Kahama, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Mikocheni B jijini Dar es Salaam,leo chana kwa ajili ya kutoa pole. 
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani hapo
 Bakari Mwapachu pia akiwa msibani hapo
 Mama Anne Makinda akiwafariji wanafamilia
Mama Anne Makinda akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.