Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI

Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika BERAK (katikati) akimtambulisha Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi huo Bi. Beatrice Alperte (kushoto) kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika BERAK aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika BERAK(katikati) pamoja na Mshauri wa Uchumi wa Ubalozi wa Ufaransa Bi. Beatrice Alperte (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam. 
Balozi wa Ufaransa alimueleza Mhe. Makamu wa Rais juu ya Kongamano kubwa la Biashara litakalofanyika Dar es Salaam mwezi Aprili, Kongamano hilo litajumuisha makampuni 50 kutoka Ufaransa.
Lengo la Kongamano hilo ni kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.