Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS WA SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI SADC

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo March 18,2017 amehudhuria mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC  akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.  Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mfalme Mswati wa III wa Swaziland mjini Mbabane Swaziland ambae amezitaka Nchi wanachama wa SADC kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jumuiya hiyo kama hatua ya kuwakwamua  wananchi na umasikini.
 Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefunguliwa rasmi leo na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mfalme Mswati III wa Swaziland ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe –Swaziland.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dakta John Pombe Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) watajadili mambo mbalimbali yanayolenga kuimarisha utendaji kazi wa Jumuiya hiyo hasa katika sekta za viwanda, elimu, miundombinu, mtangamano wa masoko, ulinzi na usalama pamoja na kuweka mfumo wa kushirikisha sekta binafsi katika ngazi zote za utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwenye jumuiya hiyo.

Akifungua Mkutano mkutano huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika Mfalme Mswati III wa Swaziland amezitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuimarisha mipango na mikakati inayolenga kuhakikisha wananchi wa nchi za jumuiya hiyo wanapata huduma bora za kijamii.
Mfalme Mswati III amesema nchi wanachama wa SADC zikishirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Jumuiya hiyo anaimani kuwa tatizo la uhaba wa ajira na umaskini litapungua kwa kiasi kikubwa kwenye nchi hizo.

Ameeleza kuwa ili nchi wanachama wa SADC ziweze kuimarisha shughuli za uchumi ni muhimu kwa mkakati wa kuendeleza na kujenga viwanda ukatiliwa mkazo kwa sababu nchi hizo zina rasilimali nyingi ikiwemo madini, mifugo na masuala ya utalii.
Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) watajadili mambo mbalimbali yanayolenga kuimarisha utendaji kazi wa Jumuiya hiyo hasa katika sekta za viwanda, elimu, miundombinu, mtangamano wa masoko, ulinzi na usalama pamoja na kuweka mfumo wa kushirikisha sekta binafsi katika ngazi zote za utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwenye jumuiya hiyo.
Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya wataalamu, Makatibu Makuu na Mawaziri wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Mawaziri unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga akisaidiana na Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.
Katika ngazi ya Makatibu Wakuu ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Balozi Aziz Mlima Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mbabane- Swaziland.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.