Habari za Punde

MARAIS, VIONGOZI WASTAAFU WAONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA BALOZI SIR GEORGR KAHAMA DAR

 Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo. Kulia kwao ni Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. 
 Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal,  wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
 Waziri wa Habari  Utamaduni , Sana na Michezo, Nape Nnauye, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakatia wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es  Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwafariji baadhi ya wanafamilia ya marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini. 
 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe (kushoto) Prof. Rwekaza Mukandalana Spika wa Bune mstaafu, Anne Makinda, wakiwa msibani hapo.
 Makamu wa Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhman Kinana,wakiwa katika shughuli hiyo ya msiba. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Baadhi ya wanafamilia wa marehemu Balozi Sir George Kahama.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin  MKapa, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo. 
 Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuagwa mwili wa marehemu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere. 
 Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Balozi Sir George Kahama, wakati wa shughuli za kuagwa mwili wa marehemu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere. 
 Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda (kushoto) akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Ackson Tulia, wakati wakiwa katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu Balozi Sir George Kahama katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.