Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA STARS NA BURUNDI LEO TAIFA

 Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mbaraka Abeid (katikati) akidhibitiwa na mabeki wa Burundi wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Stars ilishinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Simon Msuva kipindi cha kwanza na Mbaraka Abeid kipindi cha pili.
 Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Tanzania. Taifa Stars, Faridi Mussa, akijaribu kupiga shuti huku akizongwa na beki wa Burundi (chini) wakati wa  mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Simon Msuva, akichuana kuwania mpira na beki wa Burundi, Hererimana Rashid, wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Chenga ya mwili.............................
Mavugo akichanja mbuga

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.