Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA YANGA VS ZANACO JANA

Simon Msuva akimchambua kipa wa Zanaco na kuifungia timu yake bao.
Na Ripota wa Mafoto Blog Dar
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa AFrika, Yanga SC, leo wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Zanaco kutoka nchini Zambia katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Baada ya sare hiyo Yanga watahitaji ushindi katika mcheozo wa ugenini wa marudiano wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Zambia. 
Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Simon Msuva katika dakika ya 39 akimalizia pasi ya mwisho ya Justine Zulu na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza.
Yanga watajilaumu kwa kukosa mabao mawili zaidi ya wazi katika 
dakika 15 za kuelekea mwisho wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Yanga walianza tena kutumia mipira mirefu ya kutokea pembezoni mwa Uwanja kujaribu kulazimisha mashambulizi langoni mwa Zanaco, lakini safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Zambia ilikuwa imara kudhibiti.
Zanaco walisawazisha bao hilo dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame aliyetumia mwanya wa mabeki wa Yanga kuzubaa kusubiri wapinzani wao watoe nje mpira kiungwana (Fair Play) baada ya mchezaji mwenzao, Obrey Chirwa kuangushwa.
Kwame alifunga mbee ya mabeki wa kati watatu wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan na Vincent Bossou na kipa wao Deogratius Munishi ‘Dida’ baada ya krosi kutoka wingi ya kulia.
Bao hilo lilionekana kabisa kuwavunja nguvu Yanga na baada hapo wakaanza kucheza ili kumalizia mchezo kwa sare na si kutafuta ushindi.

 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.