Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA,HABARI KAMILI MTANANGE WA TAIFA STARS VS BOTSWANA

 Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania Taifa Stars, Mbwana Samatta, akifunga bao la kuongoza katika dakika ya 2 kipindi cha kwanza.
********************************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog,Dar
Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta yameiwezesha timu ya Taifa kupata ushindi  dhidi ya Botswana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofchezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaa, leo jioni.
Samatta anayechezea timu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi kuu ya Ubelgiji alifunga bao la kwanza katika dakika ya pili baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Botswana na kuupachika mpira upande wa kushoto wa kipa wa timu yaTaifa ya Botswana, Kabelo Dambe.
 Wachezaji wa Stars, Wakishangilia na kumpongeza Samatta.
 Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe, akisalimiana na Naodha wa Timu ya Taifa Taifa Stars, kabla ya kuanza mchezo huo.
*****************************************************************
Samatta aliongeza bao la pili katika dakika ya 87 kwa mpira wa faulo baada ya  kufanyiwa madhambi na Kabelo Seakanyenga na mchezaji huyo nyota, akapiga faulo ya kifundi na kumfunga tena Dambe ambaye hakuwa na la kufanya, katika dakika ya 87.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa kocha mkuu wa mpya timu ya Taifa, Salum Mayanga, tangua ateuliwe kurithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa.
Botswana ilianza mchezo kwa kasi na kufanya mashambulizi mfululizo katika dakika ya kwanza, hata hivyo wakajikuta wapachikwa bao la haraka haraka kwa staili ya ‘counter attack’ baada ya kazi nzuri ya Shiza Kichuya na Simon Msuva.
 Aliyekuwa Waziri wa habari, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, akisalimiana na mashabiki waliofika uwanjani hapo kushuhudia mchezo huo, huku wengi wakiomba kupiga naye picha ya ukumbusho
*******************************************************************
Botswana walijitahidi kutafuta bao la kusawazisha, lakini ngome imara ya Stars chini ya Abdi Banda, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein na kipa wao, Aishi Manula waliokoa hatari zote.
Bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza. Botswana iliingia kipindi cha pili ikiwa imebadili kikosi chake. kwa kiasi kikubwa. Kocha Peter Butler aliingiza vijana wenye kasi zaidi kwa lengo la kusawazisha na kuikuta Stars imara idara zote.
 Samatta, akimiliki mpira
 Faridi Mussa,akiambaa na mpira.
 Wachezaji wa Stars wakishangilia bao la Samatta la pili
**********************************************************************************
Pamoja na kufanya mashambulizi mengi na kushindwa kutumia nafasi za wazi, Botswana walipachikwa bao la pili katika dakika ya 87 kupitia kwa Samatta.
Kocha wa Stars, Salum Mayanga alisema kuwa bado anakijenga kikosi chake na kuahidi makubwa zaidi katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Burundi utakaochezwa kwenye uwanja huo huo.
Kazi bado pevu, tunatakiwa kuwapa moyo wachezaji hawa ili kuendelea kufanya vizuri na kupandisha kiwango chetu cha Fifa. Tupo katika kujenga timu na Botswana ni timu bora,” alisema Mayanga.
Kwa upande wake, Samatta alisema kuwa wanahitaji sapoti zaidi katika timu yao ili kuwaongezea morali.
 Sehemu ya mashabiki wa Taifa Stars

 Mashabiki wa Soka wakimshangilia Nape baada ya kumuona akitembea jukwaani hapo kusalimia mashabiki

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.