Habari za Punde

MEYA CHAUREMBO KUKIMBIA NA DAR JOGGING JUMAPILI MACHI 26, 2017

Klabu ya Dar Jogging imeandaa mbio za pole zitakazofanyika siku ya jumapili ya tarehe 26. Machi, 2017. Mbio hizo zitaanzia uwanja wa Taifa kuelekea Temeke Mwisho, Sudan, majaribio hadi uwanja wa Mwembe Yanga. Mbio hizo zitaongozwa na Mshahiki Meya wa Temeke ndugu Abdallah Chaurembo akiambatana na Mbunge wa Temeke Abdala Mtolea, baadhi ya madiwani kama Diwani Benjamin Ndalichako wa Kata ya Chang’ombe, na wenyeviti wa serikali za mitaa kama Mwenyekiti wa Serikali ya mitaa ya Chang’ombe Ali Majata.
Bonanza hili la jumapili linafanyika chini ya mwavuli wa Umoja wa Vilabu vya jogging vya Upatu kwa kifupi UVIJO. Vilabu vilivyoko chini ya uvijo ni pamoja na Dar Jogging, Dovya jogging, Temeke Family, Tupo Jogging, vilivyoko katika wilaya ya Temeke. Vilabu vya uvijo vinavyotoka Kinondoni ni pamoja na Barafu Jogging, Mzimuni Jogging, na Tunajenga Jogging. Madhumuini ya vilabu vya Uvijo ni kufanya mazoezi pamoja kila mwezi mara moja huku wakichangiana pesa zinazopokelewa na klabu moja kila mwezi. Mtindo huu ulioanzishwa na vilabu hivi ni kama vile mtindo ambao watu wengine wanafanya katika kuchangiana pesa maarufu kwa jina la upatu, lakini vilabu hivi vinajikita zaidi kusaidiana kiuchumi na kupeana mawazo ya nini cha kufanya hasa uendeshaji wa vilabu kiuchumi.
Vilabu vingine vitakavyokuwepo katika mbio hizo ni pamoja na vilabu vinavyounda Uvijo ni pamoja na Ferry Jogging, Haipotei Jogging, Solidarity Jogging, Faita Jogging, Zebra Jogging, Soko Mjinga Jogging, Mtoni Jogging, Mtongani Jogging, Kongowe Jogging, Serengeti Jogging, Yombo City Jogging, New Heroes, Msakala Jogging, Na Buza Joggging.
Wengine ni Waasisi Jogging, Kata 14 Jogging, Capela Bay Jogging, Mzalendo Jogging, Washikaji/Kiujamaa Jogging, Denish Jogging, Afya na Uchumi Jogging, Darajani Jogging, Matosa Jogging, Ukonga Jogging, Hananasifu Jogging, Luwanga Jogging, Luwanga Jogging, Team Pamoja Jogging, Pamoja Zaidi Jogging, Class Jogging, TEmeke Jogging, East West Jogging, Amani Jogging, Mshikamano Jogging, Ukwamani Jogging, Ambushez Joigging na Fanja Jogging.
Hatua hii ya kufanya mazoezi ya kivikundi ni hatua mojawapo ya kuunga mkono agizo la Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluh Hasan tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders. Mwenyekiti wa Klabu ya Dar Jogging ameomba vikundi vingine na wananchi kiujumla kuja kujumuika na Dar Jogging katika Bonzanza hili. Ndani ya makundi haya kuna wanamichezo mbalimbali wapo kutoka michezo mingine ikiwemo kuogelea, mpira wa miguu, netiboli, wavu, riadha na ngumi. Tunawaomba watu wote waje kukimbia na sisi na wala hauhitajiki kulipa kitu chochote.
Mwenyekiti Namkoveka aliongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na kupata kibali kutoka kwa afisa utamaduni na michezo na wenzetu wa Radio Times watajumuika nasi katika mbio hizo zitakazoishia Mwembeyanga. Baada ya mbio hizo kufanyika mechi ya mpira wa miguu kati ya Times Fm Radio pamoja na Dar Jogging mechi ambayo itafanyika katika uwanja huo huo wa Mwembeyanga.

Ramadhan Namkoveka
Mwenyekiti
Dar Jogging and Sport Club

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.