Habari za Punde

MFUMO WA MANUNUZI YA UMEME KUPITIA LUKU KUZIMWA JUMAPILI HII

NA K-VIS BLOG
SHIRIKA la Umeem Tanzania, (TANESCO), linawataarifu wateja wake na umma kwa ujumla kuwa Jumapili Machi 19, 2017 kuanzia saa 4 usiku mfumo wa ununuzi wa umeme kupitia LUKU utazimwa hadi Jumatatu Machi 20, 2017.
Taarifa ya TANESCO iliyotolewa leo Machi 17, 2017 na kusambazwa kwa vyombo vya habari imesema, lengo kuboresha mfumo huo wa LUKU katika kuhifadhi taarifa za Wateja, (Database).
Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu pia imesema uboreshwaji wa mfumo huo utasaidia katika manunuzi ya umeme kupitia LUKU.
Aidha TANESCO imewaomba Wananchi hususan wateja wake , kufanya manunuzi ya LUKU ya kutosha kabla ya saa 4 usiku, Jumapili, na inawaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.