Habari za Punde

MSAKO UMEANZA,MASHINE KADHAA ZA KUTENGEZA POMBE YA VIROBA ZAKAMATWA

Mashine zinazotumika na kiwanda cha Afro African Company kuzalisha pombe kali aina ya Viroba pamoja na kutengenezea vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe hizo
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja wa Wamiliki wa kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya viroba. Ofisi ya Makamu wa Raisi inaongoza msako wa ukaguzi wa viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha na kutengeneza pombe kali (viroba) na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.
Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha waandishi wa habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba) inayozalishwa na kampuni hiyo pasipo kufuata kanuni za TFDA wala pasipo kuweka stika za TRA.
Mrundikano wa maboksi uliopo kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za aina mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuuza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.