Habari za Punde

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR NDG. VUAI ALI VUAI ZIARANI KUIMARISHA UHAI WA CHAMA VISIWANI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai Akizungumza na Watendaji , Viongozi na wafuasi wa chama hicho katika mwendelezo ya ziara ya kuimarisha uhai wa Chama kuelekea uchaguzi wa taasisi hiyo na jumuiya zake Katika Jimbo la Jang’ombe iliyofanyika katika Tawi la Matarumbeta.
Na Is-Haka Omary, Zanzibar. 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai amewasihi vijana wa Chama hicho kuwania nafasi za uongozi katika ngazi za mashina hasa Ubalozi wa Nyumba kumi ili kuongeza nguvu za kiutendaji katika ngazi hizo. 
Amesema nafasi hizo kwa kiwango kikubwa zimekuwa zikishikiliwa na Wazee ambao umri wao hauwaruhusu kuendelea kuhudumu katika uwanja wa mapambano ya kisiasa kwa sasa. Akizungumza Naibu Katibu Mkuu huyo na viongozi, 
Watendaji na Wanachama wa Jimbo la Jang’ombe katika mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama iliyofanyika katika Tawi la CCM Matarumbeta Unguja. 
Vuai alisema nguvu za taasisi hiyo zinaanzia katika ngazi za chini za uongozi zinazotakiwa kusimamiwa na viongozi vijana wenye uwezo wa kupigania maslahi taasisi hiyo bila ya woga.
“ Kwa miaka mingi kila ukifika uchaguzi wa Chama na Jumuiya zake wanaojitokeza kuwania ngazi za ubalozi wa nyumba kumi ni Wazee na watu ambao umri wao unaelekea katika utu uzima, ambapo vijana mnazikimbia nafasi hizo na kugombea nafasi za juu wakati ngazi za chini hazina watu wenye nguvu wa kuzisimami”.alisisitiza Vuai na kuongeza kuwa mtaji wa kisiasa wa CCM ni wanachama hai wanaopatikana kupitia ngazi za Matawi na Mashina.
Alieleza kuwa Wazee kwa sasa wanatakiwa kupumzika huku wakipewa fursa za kushauri masuala mbali mbali ya kisiasa ndani ya taasisi hiyo, kwani wao ndio mashujaa wanaostahiki kupewa heshima kutokana na mshango wao wa kufanya mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyoleta ukombozi wa kudumu kwa Wazanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.