Habari za Punde

NAPE AAGA, AWATAKA WANANCHI KUKUBALIANA NA MAAMUZI YA RAIS DKT. MAGUFULI

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliyetangazwa leo kuenguliwa katika nafasi hiyo, na mbunge wa Mtama, Nape Mosses Nnauye, amewataka Watanzania kutokuwa na jazba na badala yake kukubaliana na maamuzi yaliyofanywa na Rais ya kutengua uteuzi wake wa Cheo alichokuwa nacho na kumtagaza Waziri Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana nje ya Hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay jijini Dar es Saam, Nape alisema kuwa yeye binafsi amekubaliana na maamuzi ya Rais, na kusema kuwa, anashukuru kwa hapo alipofikia na kuweza kufanya kazi na Rais Magufuli.
Nape alifikia hatua hiyo ya kuzungumza na wanahabari nje ya Hoteli hiyo baada ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro, kufika eneo hiyo na kuweka zuio la kufanya mkutano huo, huku Nape akiwatangazia waandishi watawanyike eneo hilo na kuendelea na shughuli zao.
''Ili kunisaidia mimi nawaombeni mtawanyike mahala hapo na muendelee na shughuli nyingine na mimi niende zangu kwangu, na Kamanda Siro si mnamuona huyooo anaondoka zake''.alisema Nape kuwatangazia waandishi wa habari waliokuwa wamekusanyika eneo hilo wakisubiri azungumze.
Nilipenda kuendelea kufanya kazi nanyi lakini muda wa aliyeniteua umefikia tamati, nitawakumbuka sana, ninawapenda sana ila ninawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe na kuendelea kumwamini Rais wetu John Pombe Magufuli kwani ndiye tuliyepewa na mungu, ndiye rais tuliyemchagua,” amesema Nape.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.