Habari za Punde

NEY WA MITEGO ALIPOACHIWA HURU KUTOKA KITUO CHA KATI LEO MCHANA

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, aliyekuwa amekamatwa na kushikiliwa na maafisa wa polisi nchini, baada ya kutoa wimbo wake mpya uitwao 'WAPO'. 
Ney wa Mitego ameachiliwa huru kufuatia uamuzi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kupokea ushauri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli,kuwa aachiwe huru na kumpa ushauri kuboresha muziki wake kwa kuongeza baadhi ya mambo.
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita na kukamatwa jana huko maeneo ya Morogoro na kuletwa jijini.
Katika taarifa yake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema kuwa mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.