Habari za Punde

RAIS WA CHEMBA YA BIASHARA, VIWANDA NA KILIMO AHIMIZA WATANZANIA KUTUMIA FURSA YA SOKO LA AWALI

Rais wa Chemba ya Biashara,viwanda na kilimo, Ndibalema Mayanja, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mikoa ya Mwanza na Kagera kuchangamkia soko la awali la hisa za TCCIA Investment PLC.
Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa mikoa hiyo bwana Mayanja alisema “TCCIA Investment PLC ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja, imara na inafanya vizuri sana kwani tangu ianzishwe mwaka 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97 imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 na imekuwa ikilipa gawiwo kwa wanahisa wake. Hii ni fursa muhimu na adhimu muitumie kabla ya tar 14 mwezi huu March. “ alisema Mayanga
Rais huyo wa Chemba akiwa ziarani mkoani Mwanza na Kagera pia alifanya kazi ya kujenga uhai wa chemba kwa kukutana na viongozi mbalimbali katika mikoa hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.