Habari za Punde

SAMATTA AZIDI KUNG'ARA ULAYA ATUPIA MAWILI GENK IKISHINDA 5-2

Mshambuliaji wa Kimataifa Mtanzania, Mbwana Samatta ameibeba timu yake  baada ya kuifungia timu yake mabao mawili kati ya matano wakiwa ugenini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora UEFA Europa League.
Katika mchezo huo uliofanya Uwanja wa Ghelamco- Arena mjini Gent, Samatta alifunga mabao yake dakika za 41 na 72, wakati mengine ya wageni yalifungwa na kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 21, mabeki Mgambia Omar Colley dakika ya 33 na Mfinland Jere Uronen dakika ya 45.
Samatta (kulia) na beki Mgambia Omar Colley wakisujudu baada ya kufunga.
*******************************
Mabao ya wenyeji yalifungwa na mshambuliaji kutoka Nigeria, Samuel Kalu Ojim dakika ya 27 na mshambuliaji kutoka Mali, Kalifa Coulibaly dakika ya 61 na sasa Genk watakuwa na mchezo mwepesi wa marudiano nyumbani kuwania Robo Fainali.
Samatta jana amefikisha mabao 16 katika mechi 47 alizoichezea Genk tangu asajiliwe Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC.
Kati ya mechi hizo 47, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 29 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 28 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 18 msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na tisa msimu huu na katika mabao hayo 16, 10 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.