Habari za Punde

SIMBA YALAZIMISHA SARE YACHOMOA JIOOOOONI KWA MBEYA CITY


TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo almanusura izame mbele ya 'Wagonga nyundo' Mbeya City baada ya kutangulia kufungwa bao la kwanza na la pili huku wao wakifanya kazi ya kusawazisha.
Baada ya mchezo huo wa leo sasa Simba wamefikisha jumla ya pointi 55 wakiwa wamecheza mechi 24, wakiambulia pointi moja tu leo huku watani zao wakishuka dimbani Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kesho kukipiga na Mtibwa Sugar, huku wakiwa na Pointi 52 na wakiwa wamecheza echi 23.
Kwa matokeo hayo SImba wamepunguzwa kasi ya kumkimbia mtani wake Yanga ambapo iwapo Yanga ataibuka na ushindi katika mchezo wa kesho basi watakuwa na Pointi sawa, wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Mbeya City wao baada ya sare leo, wanafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 24. 
Hadi mapumziko Mbeya City walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 37 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya Raphael Daudi.
Hajib aliisawazishia Simba SC kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 65, uliopigwa nje kidogo ya boksi la Mbeya Ciry baada ya Bryson Raphael kuunawa mpira.
Baada ya bao hilo, Mbeya City walikuja juu na kusaka bao lakuongoza ugenini na walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 79, mfungaji Nahodha wake, Kenny Ally.
Hata hivyo, Simba SC wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Shiza Kichuya aliyefunga kwa penalti dakika ya 86 baada ya Tumba Lui kumuangusha beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye boksi.

KATIKA MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LIGI KUU NI: 
Toto Africa 2- Mbao Fc 0
Kagera Sugar 1 - Majimaji 0

Simba 2 - Mbeya City 2

Mchezo wa Azam vs Stand Utd unaendelea muda huu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.