Habari za Punde

TAIFA STARS YATAKATA BILA SAMATTA, YAICHAPA BURUNDI 2-1

 MABAO mawili ya kila kipindi yaliyofungwa na washambuliaji, Simon Msuva na Mbaraka Abeid yalitosha kuipa ushindi  wa mabao 2-1 Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ dhidi ya Burundi, katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,jioni ya leo.
Ushindi huo ni wa pili ndani ya siku tatu baada ya Jumamosi iliyopita kuifungaa timu ya Taifa ya Botswana kwa bao 2-0.

Katika mchezo wa leo, Stars ilimkosa nahodha wake, Mbwana Samatta ambaaye alicheza kwenye mchezo wa Jumamosi na kuiwezesha Stars kuibuka na ushindi huo wa mabao  mawili ambayo yote yalifungwa Samatta.
Stars ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Msuva aliyetumia vizuri pasi safi ya kichwa kutoka kwa Ibrahim Ajib.
Stars ambayo haikuwa kwenye ubora wake ukilinganisha na mchezo uliopita, iliwapumzisha baadhi ya wachezaji wake waliocheza mchezo uliopita.

Stars ilienda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 lakini iliwachukua Burundi dakika nane tu tangu kuanza kwa kipindi cha pili kusawazisha bao hilo kupitia kwa Laudit Mavugo aliyetumia vizuri makosa ya beki wa kati wa Stars, Abdi Banda.
Kinda aliyetokea benchi, Mbaraka Abeid, kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Farid Mussa, aliwainua tena mashabiki wa Stars kwa kutupia bao la pili baada ya kuuwahi mpira uliopigwa kutoka nyuma na kumchambua kipa wa Burundi na mpira kugonga mwamba kabla haujamrudia tena Mbaraka na kuukwamisha wavuni.

Matokeo ya Mchezo huo wa Kimataifa wa kirafiki, huenda yakaipandisha  Tanzania kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la soka Duniani (FIFA). KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA ZA MTANANGE HUU KAA NASI HAPO BAADAYE.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.