Habari za Punde

TANESCO YATOA TAARIFA YA KATIZO LA UMEME SEHEMU KUBWA YA JIJI KESHO MACHI 26

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala jijini Dar es Salaam, kitakuwa kwenye maboresho makubwa Machi 26, 2017 na hivyo itapelekea eneo kubwa la jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Bi. Leila Muhaji imesema umeme utakosekana kuanzia saa 3 asubuhi na kurejea saa 10 jioni ambapo ametaja maeneo yatakayoathirika kufuatia kazi ya kuboresha kituo hicho ni pamoja na eneo la katikati ya jiji, Upanga, Kariakoo, Buguruni, Ilala, Mbagala na Chang’ombe.
Aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Kurasini, Kiwanda cha saruji Maweni, Wizara ya Maliasili na Utalii, (Mpingo House),Tusiime Mission na Tanzania Oxygen. Mengine yaliyotajwa ni pamoja na Ofisi ya Manispaa ya Temeke, Unilever, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jarmana Printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate, na maeneo jirani.
Bi. Leila aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na Goldstar, Quaim, Robbarac, Simba Plastic, Veta, Duce, JKT Mgulani Barracks, Keko, Mkuranga,Chuo cha Diplomasia, 21st Century, Oilcom, Engen na eneo la Mtoni Mtongani.
Aidha kufuatia katizo hilo la umeme, TANESCO imetoa tahadhari kwa wananchikutoshika nyaya za umeme zilizokatika na kwuataka watoe taarifa kwenye namba za dharura za TANESCO.
Leila alisema, uongozi wa TANESCO unaomba radhi kutokana na usumbufu utakaojitokeza kutokana na kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.