Habari za Punde

TANZANIA KUWA SALAMA KATIKA MATUMIZI YA MITANDAO.

Na: Frank Shija – MAELEZO.
USALAMA wa mitando “Cyber Security” ni jambo muhimu la kutiliwa mkazo hasa katika zama hizi za kidigitali kwa kuwa uwepo wa usalama  katika matumizi ya mitandano ni sawa sawa na kuhakikishia dunia usalama duniani kote.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magezeti ya Daily News, Habari Leo na Spoti Leo Dkt. Jim Yonaz wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma, Idara ya Teknolojia ya Habari kwa lengo la kufanya majadiliano na kuonyesha matokeo ya utafiti kuhusu mifumo ya kuhakikisha Usalama wa mitandao leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Yonazi amebainisha kuwa zaidi ya watu milioni 18 ni watumiaji wa huduma ya mtandao (internet) idadi ambayo ni kubwa hivyo ni muhimu sana kuweka namna sahihi ya kulinda usalama wa watumiaji hao.
“Nashauri pia katika utafiti wenu mkiendelea kuboresha mbinu hizo za kuhakikisha uaslama katika matumizi ya mitandao hakikisheni mnaweka kipengele cha kumuepusha mtoto na madhara ya matumizi mabovu ya mitandao,” alisema Dkt. Yonaz.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Utafiti kuhusu Mradi wa Usalama wa Mitandao kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Leonard James Mselle alisema kuwa warsha hiyo ni hatua muhimu kwani inakwenda kudhihirsha namna ambavyo Tanzania imejipanga katika kuhakikisha matumizi ya mitandao yanakuwa salama.
Profesa Mselle alisema katika warsha hiyo watafiti wataonyesha mifumo wa kuhakiki uhalali wa taarifa zinazopitia kwenye mitandao ambayo imebuniwa na wataalam wa Teknolojia ya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.
“Katika warsha yetu leo tunakuja kuonyesha mfumo ambao utakuwa na uwezo wa kubaini taarifa au picha iliyochakachuliwa hivyo mfumo ambao unatuhakikishia usalama katika matumizi ya mitandao,”alisema Profesa Mselle.
Warsha hiyo ni matokeo ya mpango ulioasisiwa mwaka 2013 na Mamalaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA)kwa kushindanisha wadau kuandika makala juu ya Usalama wa Mitandao ambapo UDOM walishiriki na kuibuka washindi wa andiko lililopelekea kufanyika kwa utafiti wa namna ya kuhakikisha usalama wa kutumia mitandao kuwasilisha taarifa mbalimbali. Utafiti huo umebaini mbinu ya namna ya kubaini taarifa zilizoharibiwa kutoka kwenye uhalali wake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.