Habari za Punde

TANZANIA YAONGOZA KWA KASI NDOGO YA ONGEZEKO LA MFUMUKO WA BEI KATIKA AFRIKA MASHARIKI.

 Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na waadishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Februari 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtakwimu kutoka Ofisi hiyo Hashim Njewele.
 Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na waadishi wa habari kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Februari 2017 leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo kuhusu hali ya mfumuko wa bei kutoka kwa Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi ha oleo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
*******************************************************************
Na: Frank Shija – MAELEZO.
Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania umeongezeka kwa kiasi kidogo ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Februari mwaka 2017.
Ruth amesema kuwa mfumuko huo umeongeka kutoka asilimia 5.2 mwezi Januari hadi kufikia 5.5 mwezi Februari, 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.3 kiasi ambacho hakina athari katika uchumi wa nchi.
“Ongezeko hilo la mfumuko wa bei umeendelea kukua kwa kiasi kidogo ukilinganisha na nchi zingine za ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo Uganda na Kenya ambazo tunashabihiana kwa kiasi kikubwa”. Alisema Ruth Minja.
Kwa upande wa mfumuko wa bei kwa bidhaa za Vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka, umeongezeka hadi asilimia 9.3 kutoka asilimia 8.2 mwezi Januari, 2017, wakati badiliko la fahirisi kwa bei zisizo za vyakula limebaki kuwa asilimia 3.6 kama ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.
Ameongeza kuwa farihisi za bei zimeongezeka hadi 106.97 mwezi Februari,2017 kutoka 101.44 mwezi Januari, 2017 wakati mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Februarii,2017 zimeongezeka hadi asilimia 8.7 kutoka asilimia 7.6 ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.
“Mwenendo wa fahirisi za bei za Taifa na Mfumuko wa Bei kutoka mwezi Februari 2016 hadi mwezi Februari, 2017 umeendelea kuimarika  ambapo katika kipindi hicho, mfumuko wa bei umekuwa na mwenendo imara kutoka asilimia 5.6 mwezi Februari, 2016 hadi asilimia 5.5 februari,2017,”alisema Kaimu Meneja huyo.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kupitia Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inao wajibu na mamlaka ya kuratibu upatikanaji na utoaji wa takwimu rasmi  nchini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.