Habari za Punde

TFF YASHINDWA KUPATA MUAFAKA, OFISI ZAENDELEA KUFUNGWA, SERENGETI BOYS KUSAKA UWANJA WA KUFANYIA MAZOEZI


 Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Katika sakata hilo ambapo timu ya Serengeti Boys ipo kambini ndani ya Shirikisho hilo, wameendelea kusalia lakini wamepewa masharti ya kutokutumia uwanja huo kwa mazoezi mpaka pale watakapomalizana na TRA.
Baadhi ya viongozi wa TFF walijaribu kwenda ofisi za TRA mkoa wa Ilala kujua ni jinsi gani wanalimaliza sakata hilo liligonga mwamba na kushindwa namna ya kujikwamua kwenye adha hiyo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeendelea kuwa katika sintofahamu baada ya ofisi zake kufungwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) baada ya kuwa na malimbikizo ya muda mrefu.
Maofisa hao kutoka kampuni ya YONO Auction Mart walipewa mamlaka na TRA ya kufungia ofisi hizo za TFF huku wakiwaambia hawaruhusiwi kuendelea na kazi mpaka pale watakapomalizana na TRA.
Kwa mujibu wa deni hilo, TFF wanadaiwa deni la nyuma ambalo lilikuwa chini ya uongozi wa Leodigar Tenga ikiwemo kodi ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Marcio Maximo na kodi ya mechi ya Taifa Stars na Brazil.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.