Habari za Punde

TRL YAZINDUA TRENI YA MIZIGO KWENDA BURUNDI

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Jumbe Kiko (katikati) akiinua bendara kuashiria uzinduzi wa safari za Treni ya mizigo kuelekea Burundi. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam. 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Jumbe Kiko (katikati) akiinua bendara kuashiria uzinduzi wa safari za Treni ya mizigo kuelekea Burundi. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. 
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KAMPUNI ya Reli Tanzania le, imezindua treni ya mizigo yenye mabehewa 20 iliyoanza kufanya safari zake kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nchi za Afrika  Mashariki, ambapo leo imeanza kwenda Burundi.
Mizigo hiyo inayotoka katika nchi za mbali na kutua  bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuisafirisha kwenda nje ya Tanzania katika nchi za jirani.
  Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Jumbe Kiko, alisema kuwa ,mabehewa hayo yamebeba  mizigo yenye malighafi ya chuma  (iron coils) inayosafirishwa na kampuni ya UBUCOM ya Burundi ambapo itachukua muda wa siku tatu kufika Bunjumbura.
“TRL imerudi katika ubora wake, hivyo wafanyabiashara wasisite kusafirisha mizigo yao kwa usafiri wa treni hiyo yenye ubora na bei nafuu”alisema Kiko.
Aidha Kiko, alisema mzigo uliosafirishwa hii leo umetokea nchini China ambao ulitua katika Bandari ya Dar es Salaam na TRL wanausafirisha kwenda nchini Burundi.
Kiko alisema hapo awali walikuwa hawana huduma hiyo lakini hivi sasa uboreshaji katika kampuni hiyo imesaidia kuwepo kwa huduma ya usafirishaji wa mizigo kwenda nchi za jirani.
Maboresho hayo pia yatasaidia mizigo ya wateja wao kufika kwa wakati kwa kuwa mabehewa na mashine zote hufanyiwa service kabla ya kuanza safari.
Aidha alisema hivi sasa  TRL imepunguza gharama za usafirishaji wa mizigo ya kawaida (loose cargo)na ile inayohifadhiwa kwenye makasha kwenda Burundi.
TRL inatoza jumla ya dola za Kimarekani 3,056 kwa behewa moja la mizigo ya kawaida ambayo sawa na zaidi ya sh. milioni 6.5 kwa fedha ya kitanzania, kwa mizigo iliyofungashwa katika makasha hadi Bunjumbura Burundi ni dola 3024 sawa na zaidi ya sh. milioni 7 kwa fedha ya kitanzania.

Alisema gharama hizo zinahusu uhudumiaji shehena bandarini Dar es Salaam,Kigoma na Bunjumbura na wa reli hadi Kigoma na wa meli hadi Bunjumbura.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.