Habari za Punde

WAISLAM WAKUTANA KUWEKA MIKAKATI YA KUPINGA UGAIDI DUNIANI

Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislam cha Al-Azhar Sharrif cha Misri (wa pili kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa Dini kwenye kongamano la kupiga vita uasi na ugaidi Duniani, kongamano hilo lilifanyika kwenye Hoteli ya Gintel Hills iliyopo Iringa, jana na kuhudhuriwa na M/Kiti C.C.M mkoani humo, Abedi Kiponza (aliyekaa katikati).
.**************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Iringa
KITUO cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri na Tanzania kimeendelea kufanya Kongamanao la kupiga vita ugaidi na uasi Duniani.
Kongamano hilo lilifanyika jana kwenye Ukumbi wa Gintel Hills uliopo mkoani Iringa.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mkurugenzi wa kituo hicho, Sheikh Hassan Mohamed, alisema kituo hicho kimejipanga kuhakikisha kinaiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kupiga vita ugaidi na uasi unaofanywa na baadhi ya watu wanaodhaniwa kuwa ni waislamu.
Alisema watahakikisha wanaungana na  Serikali kupiga vita vitendo viovu vinavyodaiwa kufanywa na watu waislamu.
Alisema kongamano hilo litasaidia watu kuacha ugaidi na kufuata misingi na sheria ya nchi ili kulinda amani ya nchi.
Alisema ugaidi unasababisha umwagaji wa damu za wasio na hatia na kuangamiza nguvu kazi za taifa.
Naye, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa, Abeid Kiponza aliwaahidi ushirikiano baina ya serikali na kituo hicho juu ya utulivu wa amani ya nchi.
Aidha, Kiponza alikitaka kituo hicho kuendeleza nguvu zake kwenye upigaji vita wa vitendo viovu kwa ajili ya kulinda amani ya nchi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.