Habari za Punde

WANA JOGGING NAO WAOMBA KUJIFUNZA MCHEZO WA KUOGELEA

Jogging sasa waomba kujifunza mchezo wa kuogelea
**********************************
Wanachama wa Umoja wa vilabu vya jogging (Uvijo) umeomba uongozi wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA) kuandaa mavunzo yamchezo wa kuogelea kwa vijana chipukizi.
Ombi hilo lilitolewa na wanachama wa umoja huo wakati wa tamasha kubwa la vikundi vya jogging lililofanyika hivi karibuni kwenye uwanja wa Mwembe Yanga.
Katika tamasha hilo ambalo lilianzia uwanja wa Taifa, wamia ya wanachama walisema kuwa ni wakati wa wao kuanza kujifunza mchezo huo ili kuendeleza mazoezi kwa ajili ya kuhimarisha afya zao.
Wanachama hao walisema kuwa mchezo wa kuogelea ni mzuri kwa ajili ya mazoezi ya mwili kwani uwezesha viungo vyote kutumika wakati wa mazoezi.
Mwenyekiti wa Dar Jogging, Ramadhan Namkoveka ambaye pia ni katibu mkuu wa TSA alipokea ombi hilo na kuahidi kulifisha kwa viongozi wenzake kwa akjili ya kutoewa maamuzi.
Wakati huo huo; Uvijo imeanzisha mkakati wa kuviinua kwa uchumi vikundi wanachama wake.
Mkoveka alisema kuwa kuanzia sasa Uvijo ikitoa msaada wa fedha vilabu wanachama kwa lengo la kuendesha miradi yao ya klabu, kukuza sekta ya michezo kwenye mazoezi na vifaa na pamoja na kukuza upatikanaji wa ajira ndani ya vilabu rafiki vya uvijo.
Hii ni mara pili ndani ya umoja huu ambapo mwaka jana waliweza kuichangia klabu ya Dar Jogging kiasi kama kilichochangwa mwaka huu.
Vilabu wanachama wa Uvijo ni Dar Jogging, Dovya Jogging, Tupo Jogging, Barafu Jogging, Mzimuni Jogging, Tunajenga Jogging, Wasafi Jogging na Temeke Family.
Tamasha hilo lilifanikiwa kwa msaada wa Times FM Radio, Ndanda Spring water, pamoja na huduma ya kwanza ikitolewa na G1 Security ambao walitoa madaktari pamoja na Ambulance.

Moja ya manjonjo ya wana-jogging wakati wa kufanya mazoezi. Manjonjo hayo uwasaidia kutokufikiria kuchoka.


Mwenyekiti wa Dar Jogging, Ramadhan Namkoveka akizungumza wakati wa Tamasha la vikundi vya Jogging Temeke.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.