Habari za Punde

WANANCHI BINAFSI WANAWEZA KUKOPA (MOGEJI) MORTGAGE MOJA KWA MOJA KWENYE MABENKI:MTAALAMU BoT

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WANANCHI binafsi wanaweza kwenda kwenye mabenki na kuomba mikopo ya fedha za ujenzi, (Mortgage Finance), bila ya kuanza kupitia kwenye taasisi nyingine za fedha.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi-Usimamizi wa Mabenki Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Eliamringi Mandari, (pichani juu), wakati akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa mikopo ya fedha kwa ajili ya ujenzi, (Mortgage Finance) na utunzaji taarifa mteja (mkopaji) katika kitunza taarifa cha kibenki, (Databank) kwenye semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha leo Machi 29, 2017 inayoendelea kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (tawi la Zanzibar), mjini Unguja. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
“Watu wengi hawajui kama kuna fursa hii ya ku-mortgage, kwa maana ya kujenga, kununua au kurekebisha nyumba yako, na katika kudhamiria kufanya hayo, benki inaweza kutoa masharti ambayo ni ya kurejesha fedha (mkopo) huo kwa muda mrefu kati ya miaka 5 hadi 20.” Alisema.
Hata hivyo alisema kama ilivyo kwa masharti mengine yahusuyo kukopa, hata fursa hii ya kukopa fedha kwa ajili ya ujenzi vigezo na masharti pia huzingatiwa ili benki iweze kutoa mkopo huo.
Aidha kuhusu mfumo wa taarifa unaosaidia mkopeshaji,(lender), kumjua mkopaji, (borrower), ujulikanao kama, Credit Reference System, (DBS), alisema Sheria namba 48 ya BoT kuhusu masuala ya kubadilishana taarifa za mikopo, kwa mabenki na taasisi nyingine za fedha inalazimisha mabenki na taasisi hizo kutuma taarifa za wateja (wakopaji), kwenye Databank ya BoT kila mwezi, alisema Bw. Mandari.
Alisema pia BoT, inaandaa utaratibu utakaolazimisha wakopeshaji binafsi na Taasisi za Kibinafsi, (NGOs), zinazojihusisha na utoaji mikopo, kusimamiwa, (Regulated), katika utoaji wa taarifa za mteja (mkopaji), katika kitunza taarifa cha kibenki, (Databank), ili kuwaondolea usumbufu wananchi.
“Ni kweli Sheria inaitaka Benki Kuu kusimamia taasisi za fedha zinazochukua amana kutoka kwa wananchi, kwa kuwasilisha taarifa hizo za wakopaji kwenye mfumo huo wa BoT wa Databank, lakini kwa sasa wakopaji binafsi na taasisi za hiari zinazojishughulisha na utoaji mikopo ya kifedha, bado sera inaandaliwa ili na wao waweze kusimamiwa.” Alisema.
Alisema, wakopaji binafsi na NGOs zinazojihusisha na utoaji mikopo, zimekuwa zikitumia mabavu wakati mwingine katika kufuatilia marejesho ya mikopo kutokana na utaratibu usio wazi wa kukopa, na wakati mwingine wakopaji wanarejesha mikopo kwa riba kubwa, alifafanua.
Bw. Eliamringi Mandari, akiwasilisha mada hiyo.
Meneja Msaidizi Msoko ya Ndani wa BoT, Bw.Genes Kimaro, akiwasilisha mada juu ya Majukumu ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Utekelezaji wa Sera ya Fedha wa BoT.
Bw.Genes Kimaro
Mchambuzi wa Masuala ya Fedha wa BoT, Bw.Mohammed Kailwa, (kushoto), akijibu baadhi ya hoja wakati akisaidiana na Meneja wa Masoko ya Ndani, Kurugenzi ya Masoko ya Fedha (BoT), Bw.Reverian Felix.
Baadhi ya waandishi wa nhabari za Uchumi na Fedha wanaohudhuiria semina hiyo.
Meneja wa Fedha na Utawala, Bodi ya Bima ya Amana ya BoT, Bw. Richard Malisa, akitoa mada jinsi Bodi ya Bima ya Amana inavyokinga amana za wananchi.
Mwandihi wa Clouds TV, Bw. Austin Beyadi, (kulia), akihariri habari wakati semina ikiendelea. Kushoto ni Grace Semfuko wa Star Tv.
Mmiliki wa Mtandao wa TZ Business News Online, Jaston Binala, akizungumza kwenye semina hiyo.
Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT Bw. Lwaga Mwambande, (kulia), akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina, (kushoto), akizungumza jambo na Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari Zanzibar, (ZBC), wakati wa mapumziko ya mchana ya semina hiyo.
Mwenyekiti wa Semina, ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Raia Mwema, Bw. Ezekiel Kamwaga, akizungumza kwenye semina hiyo.
Bi. Vicky Msina, (kulia), na Bw. Lwaga Mwmbande kutoka Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, BoT, wakifuatilia mijadala na mada zilziokuwa zikitolewa.
Bi. Vicky (kulIa), akiwa na Bi. Flora Mkemwa kutoka Idara ya Uhusiano na Itifaki BoT.
Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, akifuatilia mjadala.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.