Habari za Punde

WASTAAFU DAR WAANZA KUHAKIKIWA, WAGONJWA KUHAKIKIWA MAJUMBANI

Mkaguzi wa ndani, Mary Mauki (kulia) akimhakiki Agness Yaredi, mkazi wa Kibamba ambaye ni Mstaafu wa Wizara ya Elimu aliyepunguzwa kazini tangu mwaka 1996, wakati wa zoezi la kuhakiki Wastaafu lililoanza leo Machi 6, 2017 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar esSalaam.
******************************************** 
 Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga ametoa wito kwa wastaafu wanaolipwa Pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango ambao ni wagonjwa na hawawezi kufika katika viwanja vya Karimjee na Mwalimu Nyerere(Sabasaba) kwa ajili ya uhakiki wa nyaraka zao kutoa namba za simu na majina yao ili waweze kuhakikiwa pale walipo kama ni Hospitali au nyumbani.
Bw.Mohamed Mtonga ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya zoezi la uhakiki wa taarifa za wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango linalofanyika katika Jiji la Dar es Salaam kuanzia leo tarehe 6-10 Machi.
“Kwa sasa ninavyozungumza zoezi hili liko kwenye hatua ya mwisho katika Mkoa wa Dar es Salaam,Zoezi hili lilianza Mkoa wa Pwani na tumelifanya nchi nzima na limefanyika kwa ufanisi mkubwa sana na wastaafu wengi wamejitokeza na kama mnavyoona zoezi limekuwa likiendelea kwa utaratibu mzuri sana”,Aliongeza Bw.Mtonga.
Mtonga amesema wastaafu hao wengi ni watumishi wa Serikali ambao walifanya kazi kabla ya mwaka 1999 ambapo walikuwa hawapo katika mifuko ya pensheni ndio ambao wanalipwa pensheni na Serikali wakiwemo watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha amesema lengo kubwa la kuhakiki wastaafu hao ni kuboresha daftari la wastaafu ili kusaidia kujua ni kiasi gani cha wastaafu wapo katika kumbukumbu ya daftari la pensheni na kusisitiza wastafu ambao hawatajitokeza watafutwa katika daftari hilo.
Ukaguzi huu kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 na ukaanza tena mwezi Octoba mwaka 2016.
 Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA) Celina Muhingo (kulia), akimhoji, Mstaafu wakati wa zoezi la kuhakiki Wastaafu lililoanza leo Machi 6, 2017 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar esSalaam. Zoezi hilo litakuwa ni la siku tano ambapo linatarajia kumalizika siku ya Ijumaa kwa jiji la Dar es Salaam. 
 Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA) Evelyne Chande (kushoto), akimhudumia Mstaafu wakati wa zoezi la kuhakiki Wastaafu lililoanza leo Machi 6, 2017 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar esSalaam. Zoezi hilo litakuwa ni la siku tano ambapo linatarajia kumalizika siku ya Ijumaa kwa jiji la Dar es Salaam. 

 Mkaguzi wa Ndani, Emmanuel Kizigha na wenzake (kulia) wakiwahakiki baadhi ya Wastaafu waliofika katika zoezi la kuhakiki wastaafu lililoanza leo Machi 6,2017 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo linatarajia kumalizika siku ya Ijumaa. 
 Mhasibu wa Wizara ya Fedha Babu Kaguhe (kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi ya Wastaafu waliofika kuhakikiwa katika zoezi hilo lililoanza leo Machi 6, 2017 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar esSalaam.
 Mkaguzi wa ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali, Stanley Mpembe (wa pili kulia) akimjazia Fomu mmoja wa Wastaafu waliofika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 6, 2017 kwa ajili ya kuhakikiwa. Zoezi hilo lililoanza leo kwa jiji la Dar es Salaam linatarajia kumalizika siku ya Ijumaa wiki hii.
 Baddhi ya Wastaafu wakiwa katika foleni kusubiri kuhakikiwa katika zoezi hilo leo
 Baddhi ya Wastaafu wakiwa katika foleni kusubiri kuhakikiwa katika zoezi hilo leo
Baadhi ya Wastaafu wakisubiri kuhakikiwa leo.
Baadhi ya Wastaafu wakisubiri kuhakikiwa leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.