Habari za Punde

WAZIRI NAPE APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA TUKIO LILILOTOKEA CLOUDS MEDIA.

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea taarifa ya kina kuhusu chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media akiwa na walinzi wenye silaha Machi 17, 2017.
Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas  ameishukuru Kamati kwa utulivu wao na kuifanya kazi hiyo kwa utaalamu na umakini mkubwa huku jamii ikitaka matokeo kwa haraka.
Aidha Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uamuzi na maelekezo.
“Nimeipokea ripoti na ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa wakubwa zangu wao ndo wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.

Kamati aliyoiunda Mhe Waziri ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni Bw.Deodatus Balile kutoka Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi Nengida Johanes wa Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Hassan Abbas  .

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.