Habari za Punde

YANGA B YAICHAPA KIJITONYAMA UTD 2-1 MCHEZO WA KIRAFIKI

 Mshambuliaji wa Kijitonyama Utd, Rashid Said (kulia) akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Yanga B, Cleophace Sospeter, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jana jioni. Katika mchezo huo Yanga B ilishinda mabao 2-1. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Rashid akimficha Cleophace
 Rashid akimfinya Cleophace......
 Rashid akipiga katikati ya msitu wa wapinzani
 Kipa wa Yanga B, Mbaraka Jumanne akiruka kupangua shuti la Rashid.....
 Mshambuliaji wa Kijitonyama Utd, Patrick Mizengo (katikati) akichuana kuwania mpira na wachezaji wa Yanga B Yassin Saleh (kushoto) na Twaha Hashel wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jana jioni. 
 Mshambuliaji wa timu ya Kijitonyama United inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Ngazi ya Mkoa, Adam Mkunda (katikati) akichuana kuwania mpira na beki wa Yanga B Ur 20, Yassin Saleh (kulia) wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi jioni kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama. Kushoto  ni Twaha Hashel akijiandaa kutoa msaada, katika mchezo huo Yanga B walishinda mabao 2-1. 
Cleophace akichuana na Mohamed Ally 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.