Habari za Punde

YANGA YAFUNGASHIWA VILAGO HADI KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUTOKA SULUHU UGENINI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara na wawakilishi pekee wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki, timu ya Yanga, leo wameondoshwa katika michuano hiyo na timu ya Zanaco ya Zambia baada ya kulazimishwa suluhu ugenini baada ya mchezo wa awali uliopigwa jijini Dar es Salaam, kuruhusu bao la ugenini na kutoka sare ya ba0 1-1.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa wanarejea kucheza Kombe la Shirikisho wakiungana na wawakilishi katika Kombe hilo Azam Fc ambao leo nao wanatupa karata yao ugenini huko Mbabane baada ya mchezo wao wa awali kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Yanga imetolewa kwa bao la ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Yanga wataumia zaidi kwa kutolewa na Zanaco, kwani bao la kusawazisha la Wazambia hao Dar es Salaam lililopatikana dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame lilikuwa la kuotea.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.