Habari za Punde

ZIARA YA PROFESA MAKAME MBARAWA KWENYE KIVUKO KIPYA CHA MV KAZI KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAGOGONI NA KIGAMBONI

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa akikagua mojawapo ya injini ya kivuko cha MV KAZI wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu. Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.
 Muonekano wa kivuko kipya cha MV KAZI kinachotengenezwa na Kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard kikiwa katika hatua za mwisho kukamilika wakati wa ziara ya Mh.Profesa Makame Mbarawa katika eneo la ujenzi wa kivuko hicho bandarini Dar es Salaam. Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.
 Mkurugenzi wa kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard Major Songoro akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa alama za kuendeshea kivuko kipya cha MV KAZI kitakachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni. Nyuma yake ni  Dkt. Mussa Mgwatu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa akiwasili katika kivuko cha MV KAZI kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho, kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu na nyuma yao ni Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko TEMESA Mhandisi Japhet Maselle. Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.Picha na ALFRED S MGWENO – TEMESA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.