Habari za Punde

BREAKING NEEEEEWS!!! ROMA ATUA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY ANAHOJIWA MUDA HUU

Msanii wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya Hip Hop, Roma Mkatoliki, amefikishwa kituo cha polisi Oysterbay ambako anahojiwa hadi mida huu.
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya rafiki wa karibu wa msanii huyo waliopo nje ya kituo hicho, wamesema kuwa walipata tarifa kuwa Roma, amefikishwa hapo na wao kuamua kuanza safari ya kufika kitioni hapo.
Hata hivyo bado habari za uhakika kuhusu ni wapi alikokuwa na kuletwa na nani kituoni hapo hazijapatikana, kutokana na habari kuchanganya wengine wakisema eti kuwa Roma, alijipeleka mwenyewe na wengine wakisema aliletwa na askari.
Mpaka mwandishi wa habari hizi anaondoka kituoni hapo bado mahojiano yalikuwa yakiendelea huku pakiwa hakuna msemaji juu yahili hadi hapo itakapotangazwa.
Roma alipotea majuzi katika hali ya kutatanisha akiwa na baadhi ta wasanii wenzake, ambapo jana wasanii kwa umoja wao walikaa kikao na kutangaza maamuzi ya kumtafuta mwenzao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.