Habari za Punde

CHADEMA YASEMA HAITAKUBALI KUPANGIWA VIONGOZI NA CCM

KAULI hiyo imekuja baada ya jana bunge kupiga kura za hapana kwa wagombea wa CHADEMA ambao walipaswa kuwa wawikilishi waTanzania katika Bunge la Afrika Mashariki na kusema wapende wasipende nafasi hizo mbili za CHADEMA zipo pale pale, huku akitangaza kuwa chama hicho kitakwenda mahakamani kudai haki.
"CHADEMA tutakwenda kuitafuta haki pengine, kama taifa tungetegemea kupata wawakilishi na tuwe tumemaliza uchaguzi huu wa kuwapata wawakilishi wetu kwenye Bunge la Afrika Mashariki, lakini ndiyo kwanza kwa matokeo haya na kwa utaratibu huu wa upindishaji wa sheria za uchaguzi, tutakwenda mahakamani, tutaitafuta haki hii mahali pengine" alisema Freeman Mbowe
Mbali na hilo kiongozi huyo amesema ni jambo lisilowezekana kwa chama kimoja kuwapangia wapinzani kiongozi wamtakao wao.
Lawrence Masha na Ezekiah Wenje (wagombea wa CHADEMA)
*************************************
"Ni aibu kwa taifa kwamba chama kimoja kinataka kutafuta na kupitisha mgombea wa chama kingine cha upinzani, haiwezekani na haikubaliki, Spika amevunja kanuni za Bunge, sheria hazikuheshimiwa, ubabe umetumika lakini kwetu sisi ni sehemu ya mchakato wa demokrasia tutaendelea kuitafuta haki yetu". Alisema Mbowe
Kuhusu nafasi zao, Mbowe amesema, "Nafasi mbili za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki wapende wasipende ni za CHADEMA, tutakaa tutashauriana, hawawezi kueleza sababu za msingi za kuwakataa wagombea wetu. Kwa sababu wagombea wetu wana sifa, lakini tunajua huu ni mkakati wa CCM , Rais anahusika, Waziri Mkuu anahusika na viongozi wao wanahusika. Wanatumia Sheria gani kutuchagulia wapinzani wawakilishi wetu katika Bunge la Afrika Mashariki? Alihoji Mbowe. "

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.