Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA DAR CITY YAICHAPA BOKO VETERANS 3-2 KWAO

 Mchezaji wa timu ya Dar City, Shadrack Nsajigwa (katikati) akipambana kuwapita wachezaji wa Boko Veterans, Abuu Omary (kushoto) na mwenzake wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Boko Veterani mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo Dar City ilishinda mabao 3-2, yaliyofungwa na Makocha Tembele na Salvatory Edward.
 Kipa wa Dar City akionyesha umahiri wake wa kuchana msamba kujaribu kuokoa bila mafanikio.

Akida, akionyesha uwezo wake wa kusakata kabumbu huku akicheza ndombolo akiwa katika mwendo.....

Brother Tippo akimfinya beki wa Boko
 Makocha Tembele (katikati) akiwasakata wachezaji wa Boko Veterans, Godfrey Ngonyani (kushoto) na John Dilinga 'Dj Jd'.
 Hapa Shaffii sijui alijisahau kuwa alikuwa akicheza soka na kuhis alikuwa katika mchezo wa 'Sumo' naona akimlia timing mpinzani wake. KWA PICHA ZAIDI 

 Hapa hapiti mtu ukubwa dahwa.........
 Hapa ni kuosha tuuuuu
 Palikuwa hapatoshi......
 Dj Jd akiosha......
 Hupiti hapa hunijui eeeh
 Iddi Moshi akiosha....
 Papaa Joe akijaribu kuwania mpira na mpinzani, ''Arooo nakwambia riache iro rimpira''.....
 Paa Joe akiwanyasa nyasa wapinzani.....
 Brother Tippo akimkalisha beki wa Boko
 Ohoooo,mpira kausahau nyumaaaa,  
 Brothe akiosha hataki 'spoti spoti'
 Abuu Omary naye akimuotea Nsajigwa baada ya kunyanyaswa saaana....
 Benchi la Boko Veterans halina matumaini
 Benchi la Dar City matumaini kibaaaaaao....
 Kikosi cha Boko Veterans...
 Kikosi cha Dar City.....
 Dj Jd akisalimiana na wapinzani mchezo furaha
 Dilinga akiscrach soka......
   Kocha wa Boko Veterans akitoa maelekezo kwa wachezaji waake....huku povu likimtoka mweeee
 Mafoto akimpotezea 'timing' mpinzani....
 Makocha akiambaa....
 Kama abeid Mziba hapaaaaaa......
 Juma Ndambile hata soka anajua si kudhamini ngumi tuuuu....
 Salvatory Edward akitoa bonge la pande.......
Wachezaji wa Dar City wakishangilia...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.