Habari za Punde

DROO YA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO NI YANGA SC vs MBAO FC, SIMBA SC vs AZAM FC

TIMU YA Yanga ya jijini Dar es Salaam, imepangwa kukipiga na Mbao Fc katika mchezo  wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho, (ASFC) baada ya droo iliyochezeshwa leo jioni,  na Wadhamini Azam Tv huku Simba  ikipangwa  kukipiga na  Azam Fc.
Katika mchezo wa Yanga Mbao Fc watakuwa wenyeji,  jambo litakaloilazimu Yanga kusafiri hadi jijini Mwanza  katika mchezo huo wa Nusu Fainali utakaopigwa Aprili 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Nusu Fainali nyingine itakuwa ni kati ya Simba na Azam Fc, itakayopigwa April 29 kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.