Habari za Punde

HABARI DEVELOPMENT ASSOCIATION KUZINDUA KLABU ZA KUPINGA UJANGILI TANZANIA

Katibu wa Habari Development Association (HDA), Daniel Sarungi akizungumza na Waandishi wa Habari, jana, Dar es Salaam. Wapili ni Mratibu wa Uzinduzi wa Klabu za kupambana na Ujangili Tanzania, Christopher Kajituel na kulia pia ni mratibu wa Uzinduzi huo, Chaano Samson.
*************************************
Na Bashir Nkoromo
Taasisi ya Waandishi wa Habari ambao ni wanaharakati wa kupinga ujangili ya Habari Development Developmnet Association (HDA) itafanya uzinduzi rasmi wa klabu za kupinga ujangili Tanzania kwa kufanya matukio mbalimbali kwa siku tatu mjini Morogoro.
Akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, Katibu Mkuu wa Habari Taasisi hiyo Daniel Sarungi, aliyataja matukio yatakayoambana na uzinduzi huo utakaofanyika kuanzia Aprili 20 hadi 22, 2017, kuwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu tabia za Tembo na Faru ambapo Mbuga za Wanyama na Hifadhi watatoa mabanda maalum kwa ajili ya kutoa elimu hiyo na kisha washiriki kupewa fursa ya kuuliza maswali yatakayojibiwa na watalaam.
Sarugi alisema, siku itakayofuata itatumika kwa michezo miongoni mwa mabalozi wa wanyama na baadaye Wizara ya Maliasili na Utalii itatoa takwimu kuhusu ujangili ya idadi ya tembo na faru waliouawa na idadi ya kesi za ujangili zilizotolewa hukumu na zinazoendelea kusikilizwa.
Alisema, siku ya tatu ndipo utafanyika uzinduzi rasmi wa klabu za kupinga ujangili, uzinduzi ambao utafuatiwa na matembezi maalum kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu hadi Uwanja wa Michezo wa Jamhuri mjini Morogoro.
Sarungi amwakaribisha wadau na wananchi kwa jumla kufika kushiriki matembezi hayo na kwamba hakutakuwa na gharama ya ushiriki isipokuwa atakayesukumwa kushiriki atatakiwa kuwahi mapema ili kuandaliwa vifaa vya matembezi ikiwemo fulana.
Amesema, tukio hilo limeungwa mkono na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utali, PAMS Foundatuion, TBL kupitia vinywaji vyake vya Ndovu na Bavaria, Leopard Tour, Hakuna Matata Foundation na Better Dayz Co Ltd.
Ameziomba kampuni na taasisi nyingine kujitokeza kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli katika vita dhidi ya ujangili kupitia majukumu yao ya kijamii na kwamba nafasi ya udhamini wa tukio hilo bado ipo wazi.
Sarungi amesema, hatua ya kufanya harakati hizo, ni kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kukuza utalii nchini, hasa ikiwemo hatua yake ya kununua ndege hatua ambayo itaongeza idadi ya watalii kuja nchini.
"Baada ya kuona juhudi hizi za Rais na sisi kama Wazalendo tunaona ni lazima tuhimize utokomezaji wa ujangili kwa kuwa itakuwa haina maana kama watalii wataongezeka huku wanyama kama tembo na faru akiwa wametoweka", alisema Sarungi.
Alisema kufuatia ongezeko la matukio ya Ujangili imesababisha Tanzania kuwa nchi ya tatu katika makosa ya jinai barani Afrika, hivyo klabu za kupinga ujangili vimejitolea kushiriki kikamilifu katika mapambano ya kupinga ujangili ili kuhakikisha wanayama wanalindwa hasa kwa kutolewa elimu kwa jamii.
Mweka hazina wa Habari Development Association Kaimu Mzinja (aliyesimama) akijadili jambo, wakati uongozi wa Tasisi hiyo ukitangaza uzinduzi huo wa Klabu za kupinga ujangili, leo.
Sarungi na Kaimu wakijadili jambo
Viongozi wa Associan hiyo wakiwa katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali kuhusu uzinduzi wa Klabu hizo za kupinga ujangili Tanzania. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.