Habari za Punde

JESHI LA POLISI LATANGAZA VITA, MSAKO MKALI DHIDI YA WAHALIFU WAUAJI WA ASKARI WANANE

Kamishina wa Operesheni na Mafunzo ya Polisi, Nsato Marijani, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, wakati akitoa tamko kuhusu operesheni itakayoendeshwa na jeshi hilo ya kuwasaka wahalifu waliohusika na mauaji ya Askari nane katika msitu wa Jaribu Mpakani Mkoa wa Pwani juzi. Kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba 

''Tunaomba wananchi watusamehe kwa poeresheni hii tunayokwenda kuianza, kwani askari wanane ni wengi sana na hatutakuwa na msalie mtume kwa hili, wameanza sisi tunamaliza, na jana ilikuwa ni 8 - 4, lakini tukianza nawaambia mabao yetu yatakuwa ni zaidi yao'';. alisema Marijani

Aidha Marijani ametangaza kuwa eneo hilo ni marufuku waendesha pikipiki kupita zaidi ya saa kumi na moja jioni. Kaa nasi Video inakujia hivi punde

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.