Habari za Punde

KINYEREZI FAMILY YAWAKUMBUKA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA NEW HOPE SIKUKUU YA PASAKA


Wadau wa Kinyerezi Family kiwa sambamba na Watoto wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu,New Hope kilichopo Tabata,wakisali kwa pamoja mara baada ya kuwakabidhi Msaada wa vitu mbalimbali,ikiwemo mchele,nyama,sukari,mayai,nguo na vinginevyo,ili watoto hao nao wapate kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka
Kinyerezi Family wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watoto wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu cha New Hope kilichopo Tabata,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali,ikiwemo mchele,nyama,sukari,mayai,nguo na vinginevyo,ili na watoto hao wapate kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka
Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Kinyerezi Family ,Leo Joseph Manyara na Mdau wakimkabidhi sehemu ya msaada huo Mwanzilishi na Mlezi wa kituo cha New Hope Organizationi,Bi.Consoler Eliya.Kituo hicho kilichopo Tabata,jijini Dar kinalea watoto zaidi ya 150 ambapo kati yao 32 ndio huishi kituoni hapo na wengine huja na kuondoka.
Wana Kikundi cha Kinyerezi Family wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Mwanzilishi na Mlezi wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu.Consoler Eliya
Mwanzilishi na Mlezi wa kituo cha New Hope Organization, Consoler Eliya akiwashukuru wana Kikundi cha Kinyerezi Family kwa kuwakumbuka watu wenye matatizo mbalimbali kikiwemo kituo chake,kwa kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali,ili na wao waweze kusherehekea kwa furaha siku ya Pasakam,Concoler amewaomba wana Kikundi hao na wadau wengine mbalimbali kuwa na moyo wa kujitolea katika suala zima la kusaidia jamii zenye matatizo,kwani kwa kufanya hivyo hata Mungu hawaongezea zaidi palipopungua na kuendelea kuwabariki wao na familia zao.
Katibu Msaidizi wa Kikundi cha Kinyerezi Family,Michael Masota akitoa utambulisho na muongozo mfupi mara baada ya kufika kituoni hapo,kushoto ni Mwanzilishi na Mlezi wa kituo hicho cha New Hope,Bi.Consoler Eliya.
Sehemu ya msaada huo wa vitu mbalimbali
Mmoja wa wajumbe wa Kikundi cha Kinyerezi Family,Bi Lightness Kweka akizungumza machache katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hicho cha New Hope

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.