Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWAAGA VIJANA WA SERENGETI BOYS, AWAANDALIA CHAKULA CHA USIKU NYUMBANI KWAKE OYSTERBAY.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwahudumia vijana wa timu ya Taifa ya Vijana wa Tanzania Ur17 Serengeti Boys, wakati wa hafla ya chakula cha jioni alichowaandalia vijana hao nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Sa laam, jana usiku.
Viajana wakipozi kusubiri Menu......
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars
 Baadhi ya Viongozi wa timu wakiwa katika hafla hiyo.
 Makamu wa Rais akimsevia Dokta wa timu...
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwahudumia Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana U17 Serengeti Boys, Bakari Shime na Mkurugenzi wa Ufundi, Kim Poulsen, wakati wa hafla ya chakula cha jioni alichowaandalia vijana hao nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Sa laam, jana usiku. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

 Makamu wa Rais na wasaidizi wake wakitoa huduma kwa viajana hao.
 Vijana wakipiga menu.....
 Menu ikiendelea...
 Mjumbe wa Kamati ya Hamasa Beatrice Singano akitoa neno
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (kulia) akimsikiliza Nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana U17 wa Serengeti Boys, Ally Msengi, wakati akizungumza kutoa shukrani kwa niaba ya wachezaji wenzake wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Selestine Mwesigwa. 
 Picha za pamoja
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiagana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Vijana wa U17 Serengeti Boys.

Makamu wa Rais Samia Suluhu akipiga picha ya kumbukumbu na msaidizi wake wa zamani, Muhidin Sufiani.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Samia Suluhu Hassan, akiagana na Ofisa Habari wa TFF, Alferd Lucas, baada ya hafla ya chakula cha jioni. 
 Waziri Mwakyembe akiagana na Beatrice Singano kutoka Airtel.
 Omary Katanga akifurahia baraka za Mhe Makamu wa Rais.
 Waandishi wakiagana na Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakati wa hafla fupi ya chakula cha usiku ambapo aliwaalika kwenye makazi yake timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe  akizungumza wakati wa hafla fupi ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa timu ya Serengeti Boys,jana usiku tarehe 04, Aprili 2017, Oyster Bay jijini Dar es Salaam.
 Nahodha wa timu ya Serengeti Boys akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mbele Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) wakati wa hafla fupi ya kuwatakia heri Serengeti Boys ambao wanajiandaa  na fainali ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yanayotarajiwa kufanyika Nchini Gabon
 Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa timu ya Taifa ya Serengeti Boys iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi akitoa neno la shukrani kwa timu ya Serengeti Boys ambao walialikwa kwenye hafla maalum ya chakula cha jioni na Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oyster Bay, jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihudumu chakula kwa nahodha wa Serengeti Boys Issa Abdi Makamba wakati wa hafla fupi ya chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) kwenye makazi yake Oyster Bay, Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja wachezaji wa  timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) mara baada ya kula nao chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake  Oysterbay, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na wachezaji wa Serengeti Boys mara baada ya kula nao chakula cha jioni ambapo aliwaalika kwenye makazi yake  Oysterbay, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.