Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU MANISPAA YA ILALA LEO

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akifurahia jambo baada ya kupewa jibu la chemsha bongo lililokuwa sahihi kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu, baada ya kumchezesha mchezo wa mahesabu ya chemsha bongo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Elimu Manispaa ya Ilala zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akiimba sambamba na wanafunzi wa shule ya awali ya Moto mpya ya Buguruni wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Elimu Manispaa ya Ilala zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto nyuma ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Mgeule iliyopo Kata ya Buyuni Ilala.  Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akisikiliza maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu, walipokuwa wakimchezesha mchezo wa mahesabu ya chemsha bongo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Elimu Manispaa ya Ilala zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 Wanafunzi wa shule ya msingi Heritage, wakipigwa kwata kwa mwendo wa haraka wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Elimu Manispaa ya Ilala zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

 Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, akivishwa Skafu...
 Wanafunzi wa shule za msingi Ilala akipita kwa mandamano mbele y jukwaa kuu na makombe yao waliyoshinda katika michezo mbalimbali, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Elimu Manispaa ya Ilala zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Shule za Msingi za Manispaa ya Ilala Dar es Salaam, wakipita mbele ya Jukwaa la mgeni rasmi na mabango yenye ujumbe mbalimbali walipokuwa wakiandamana wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Elimu Manispaa ya Ilala zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya na baadhi ya viongozi wakisimama kupokea maandmano
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Juhudi wakitoa burudani
 Mwanafunzi Abraham Paul akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao jinsi ya kujifunza kwa kutumia Tablet. 
 Watoto wakicheza 
 Watoto wakicheza
 Wanafuzni wa Shule ya awali Mtoto Mpya, Salma Bakari (kushoto) (4) na Khadija Rajab (5) wakichezea vibao vya hesabu kujifunza kupanga namba.
 Mwalimu wa Shule ya Msingi, Mgeule, iliyopo Manispaa ya Ilala, Kata ya Buyuni, Abdul Magubika, akianda bango la wanafunzi kwa ajili ya mandamano.
Ofisa Elimu Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas, akicheza muziki wa Makhilikhili sambamba na wanafunzi wa Shule ya Msingi Umoja, waliokuwa wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Elimu Manispaa ya Ilala zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.