Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA YANGA VS AZAM JANA

 Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (kulia) akichuana  kuwania mpira na beki wa Azam Fc, Daniel Amoah , wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana. Katika mchezo huo Yanga walishindabao 1-0, lililofungwa naObrey Chirwa.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzanja Bara Yanga SC wamerejea kileleni mwa ligi hiyo bada kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Fc katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi Jonesia Rukyaa akisaidiwa na John Kanyenye na Soud Lila ulikuwa na ushindani mkubwa huku Azam wakionekana kutawala sehemu ya kiungo kwa kuwachezesha Viungo wao watatu, Himid Mao, Frank Domayo na Abubakar Salum ‘Sure Boy’.
 Azam katika dakika 45 za kipindi cha kwanza walishindwa kutumia nafasi walizopata kutokana na kutokuwa makini kwa safu yao ya ushambuliaji.
  Gor,gor gor gooor, 
**********************************
Kipindi cha pili kilianza kwa kila upande kutafuta goli la kuongoza na katika dakika ya 71 mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, aliwainuamashabiki wao baada ya kuwazidi akili na nguvu beki wa Azam Yakubu Mohamed na Kipa Aish Manula wakati beki huyo aliporudisha mpira kwa golikipa aAishi Manula, ambao haukufika kwa wakati. 
 Baada ya matokeo hayo, Yanga wanafikisha alama 56 wakiwa mbele kwa alama moja dhidi ya mahasimu wao Simba wenye alama 55 ambao nao wanashuka dimbani kukipiga na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. Leo jioni.
 Geofrey Mwashiuya akimfinya Erasto Nyini. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


 Gadiel Michael akituliza mpira gambani
 Erasto Nyoni akiufinya msitu wa wachezaji wa Yanga
 Haruna Niyonzima akimfinya beki wa Azam
 Msuva akikwepa kwanja la Himid 
 Kikosi cha Yanga dhidi ya Azam
 Kikosi cha Azam dhidi ya Yanga
 Sehemu ya mashabiki wa Azam
  Bi Harusi wa Azam aliyetua uwanjani kusubiri Bwana harusi
 WINGA wa Yanga Emmanuel Martin (kulia) akimtoka beki wa Azam Fc, Erasto Nyoni, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana. Kulia ni Deus Kaseke akisubiri kutoa msaada. 
 Hii si Kung Fu bali ni Soka.......
   Obrey Chirwa akikwepa kwanja la beki wa Azam Fc, Daniel Amoah (chini) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.
 Deus Kaseke na Erasto Nyoni
 Mashabiki wa Yanga
 Benchi la Yanga
 Heka heka langoni kwa Azam
 Niyonzima akifanya yake katikati ya wachezaji wa Azam
 Msuva akimfinya Singano
 Jamani huyu Erasto hapa anaporushia ni sahihi kweli
 Chirwa, Msuva na Martine wakishangilia bao la Chirwa.
Mwashiuya akitoka nduki na mchezaji wa Azam

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.