Habari za Punde

MBAO FC WAANGUSHA 'MBUYU' YANGA NA KUTINGA FAINALI FA KUWASUBIRI SIMBA CCM KIRUMBA

TIMU ya Mbao fc, jioni ya leo imetunga hatua ya fainali Kombe la  FA baada ya kuichapa Yanga SC kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mbao walipata bao lao kupiti kwa mchezaji George Sngita, aliyepiga krosi ambapo beki wa Yanga Vicent Andrew, akajikuta akiunganisha krosi hiyo langoni kwake katika dakika ya 26 kipindi cha kwanza.
Kwa ushindi huo sasa Mbao Fc wametinga Fainali na kuungana na Simba ambao pia waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam Fc jana katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taif jijini Dar es Salaam.
Baada ya Yanga kutolewa katika kinyang'anyiro hicho sasa wanaweka matumaini na nguvu zao zote katika michezo yao ya Ligi Kuu iliyosalia walioibuka ili waweze kutetea ubingwa wao na kupata nafasi ya kushiriki tena michuano ya Kimataifa mwakani.
Iwapo Yanga watafanikiwa kutetea ubingwa wao na kutwaa kombe la ligi Kuu, watapata nafasi hiyo huku mshindi katika fainali ya kombe la FA ndiye pia atashiriki michuano ya kimataifa huku atakayepigwa katika fainali hiyo ya FA atabaki mchangani kama alivyoaga Azam Fc jana.
Yanga watajilaumu kwa kukosa mabao kadha ya wazi kupitia kwa Amis Tambwe, Nadir Haroub na Haruna Niyonzima.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.