Habari za Punde

MECHI ZA LIGI KUU BARA KESHO, MBEYA CITY VS NDANDA FC


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo sita.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, Jumamosi Aprili 8, mwaka huu Mbeya City itashindana na Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Majimaji ya Songea itaialika African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mechi nyingine kwa siku ya Jumamosi Aprili 8, mwaka huu itakuwa ni kati ya Kagera Sugar na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera wakati wakati siku ya Jumapili Aprili 09, mwaka huu Stand United itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Ligi inatarajiwa kuendelea Jumatatu Aprili 10, mwaka huu kwa michezo miwili ambako Simba itakuwa mgeni wa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ilihali Mtibwa Sugar itaialika Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.