Habari za Punde

MGOGORO WA WACHEZAJI WAIGHARIMU YANGA IKIFUNGASHIWA VILAGO NA MC ALGERS KWA MABAO 4-0

TIMU ya Yanga iliyokuwa ikihitaji angalau  droo ili kusonga mbele katika michuano ya kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, Afrika, hatimae safari yao imeishia Algeria baada ya kukubari kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya MC Algers katika mchezo uliopigwa
mjini Al-Jaza’ir,  Algeria katika mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa awali Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 nyumbani. 
Katika mchezo huo
hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na 
Awady Said katika dakika ya 14 na 
Derraya Warid aliyefungwa na 
bao la pili katika dakika ya 39 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20.
Matumaini ya Yanga yalizdi kupotea katika kipindi cha pili, baada ya Zerdab Zahir kuifungia MC Alger bao la tatu dakika ya 66 
akitumia makosa ya mabeki wa Yanga kumuacha peke yake.
Na bao la kufunga kalamu ya mabao hayo, likifungwa 
Awady Said tena 
katika na dakika za mwisho za mchezo huo.
Dalili za Yanga kupoteza mchezo huo zilionekana mapema tu kutokana na kuibuka migogoro baina ya wachezaji na viongozi kabla ya timu hiyo kuondoka nchini juzi
.
Wachezaji wawili, beki Mtogo Vincent Bossou na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa waligoma kusafiri na timu kwa sababu ya 
madai ya mishahara yao ya miezi mitatu.
Na wachezaji kuondoka kwa ndege mbili tofauti Alhamisi likiondoka kundi la kwanza kwa ndege ya 
Emirates kupitia Dubai na kundi la pili likiondoka kwa ndege ya Uturuki kupitia Istanbul.
Kwa ujumla Yanga ilipatwa na mtikisiko wa kiuchumi tangu Februari, mwaka huu baada ya Mwenyekiti wake, Yussuf Manji ambaye 
pia ndiye mfadhili pekee wa timu kuingia matatizoni na Serikali.
Yanga iliangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia 
katika hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao ya ugenini, kufuatia sare ya 1-1 Dar es Salaam na 0-0 Lusaka.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea kesho kama kilivyokwenda kwa ndege za Uturuki na Emirates. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.