Habari za Punde

MSANII ROMA MKATOLIKI AKAMATWA HAJULIKANI ALIKO NA WENZAKE

MSANII wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya Hip Hop, Rapa Roma Mkatoliki, anayeendelea kutamba na kufanya vizuri na wimbo wake mpya wa 'Usimsahau mchizi' amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.
Habari zilizoufikia mtandao huu kupitia kwa msanii na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule 'Prof. Jay' zinasema kuwa msanii huyo alikamatwa jana majira ya jioni akiwa studio.
Aidha Prof. Jay, ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.
"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na kuondoka navyo kusikojulikana, 
Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay
Mpaka sasa bado hajafahamika wasanii hao wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. 
Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.